Wafanyabiashara stand ndogo ya Arusha wakiwa nje ya ofisi za Halmashauri ya jiji.
Awali halmashauri ilitoa viwanja kwa wafanyabiashara ikiwataka kujenga na kutumia maduka hayo kwa kipindi cha miaka kumi bila kuilipa chochote, na baadaye kukabidhi maduka hayo kwa halmashauri ya jiji.
Wafanyabiashara hao wameeleza kuwa sasa wamekuwa wakifanyabishara zao kwa wasiwasi, kufuatia mkanganyiko wa kimasilahi kati ya madalali wa maduka yao na halmashauri.
Kufuatia maelezo hayo meya wa jijji la Arusha Kalisti Lazaro akalazimika kutoa maelelekezo ya namna ya ulipaji huku akieleza kuwa tatizo kubwa ni madalali hao ambao wamekuwa wakiisababishia serikali upotevu wa mabilioni ya fedha kwa kutolipa mapato.
Mstahiki Meya amewataka wafanyabiashara hao kuendelea na majukumu yao huku akiwahakishia kuwa suala la mikataba linafanyiwa kazi katika kipindi kifupi .
Wakati mgogoro huo ukifukuta tayari duka moja limedaiwa kuvunjwa huku sababu kubwa ikidaiwa kuwa kushindwa kulipa kodi kwa halmashauri, huku muhusika akidai amelipa kodi yake yote kwa mmiliki wa wa duka hilo.
