Ijumaa , 24th Jul , 2015

Wafanyabiashara katika soko kuu la ndizi kata ya Kiwira mkoani Mbeya wanalazimika kufanyia Biashara yao ya kuuza ndizi kandokando mwa barabara kuu ya Mbeya-Kyela hadi nchini Malawi kufuatia eneo la soko hilo kuwa finyu.

Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Chrispin Meela, akimsikiliza mfanyabiashara wa ndizi katika soko la Kiwira wakati alipokuwa akikagua uendeshaji wa soko la ndizi

Aidha kitendo hicho cha wafanyabiashara hao kupanga bidhaa zao kandokando mwa barabara kimekuwa chanzo kikubwa cha kutokea kwa ajali za mara kwa mara katika eneo hilo.

Wakizungumza na chombo hiki wameeleza changamoto na adha zinazowapata wawapo sokoni hapo ikiwemo wafanyabaiashara kugongwa pamoja na ufinyu wa sehemu ya kupanga bidhaa zao.
-
Mwenyekiti wa kata ya Kiwira Joseph Mwalyambwile ameeleza jitihada zinazochukuliwa na serikali ya Rungwe ili kuweza kutatua adha hizo ikiwemo kuongea na Tanroads kuweza kuwapa eneo la hifadhi ili kujenga soko hilo.