Jumatano , 8th Jun , 2016

Wafanyabiashara Jijini Dar es Salaam wametakiwa kuendelea kuuza bidhaa zao kwa bei ya kawaida katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani na kuepuka kujiongezea faida isivyohalali kupitia mwezi huu.

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam , Alhad Mussa Salum.

Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam , Alhad Mussa Salum, ikiwa leo ni siku ya pili ya mfungo huo wafanyabiashara wengi wamesikia kilio cha waumini wa dini ya kiislam kwa kutopandisha bei kupita kiasi kwa vyakula vinavyotumika kwa futari.

Sheikh Salum amesema kuwa mwezi huu ni mwezi wa kuchuma lakini wafanyabiashara wajiepushe kuchuma visivyohalali na kuongeza kuwa endapo wafanyabiashara watazingatia hali halisi ya watanzania basi mwenyezi mungu atawazidishia zaidi ya hivi sasa.

Aidha Sheikh alhad ametumia fursa hiyo kuwataka waumini wa dini ya kiislam kudumisha amani na utulivu tuliokuwa nayo lakini na vile watumie mwezi kufanya mabadiliko ya kweli ndani ya mioyo yao.