Dkt. Magufuli ameyasema hayo wakati akihutubia wazee wa Jiji la Dar es salaam katika ukumbi wa Diamond Jublee ambapo ametumia wasaa huo kuwataka wafanyabiashara wote kuhakikisha wanalipa kodi kwa manufaa ya wananchi wote hasa wananchi wa hali ya chini.
''Serikali yangu inaunga mkono jitihada za wafanyabiashara hapa nchini na itaendelea kufanya hivyo kwa kutoa msaada wa hali na mali kwa yeyote anayetaka kufungua biashara ndogo au ya viwanda mradi tuu ahakikishe analipa kodi ili fedha hizo ziweze pia kutumika kuhudumia miradi mbalimbali ya wananchi hapa nchini'' Amesema Rais Magufuli.
Aidha Rais amewakumbusha wananchi wote kuhakikisha wanadai risiti kwa bidhaa zote watakazo zinunua iwe ni dukani au hotelini kwani bila kufanya hivyo serikali itakosa mapato ya kuendesha nchi.
Pia Rais amewataka watanzania kujenga pia utamaduni wa kujipima kama yeye wanavyo mpima kwani utasaidia kuonesha ni jinsi gani nao wanapiga hatua za maendeleo katika serikali yake ya awamu ya tano.





