Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe, Pudensiana Protas.
Kauli hiyo imetolewa wa mdau wa usalama barabarani na Mkuregenzi wa Taasisi ya Apec, Respicius Timanywa, wakati wa kufunga mafunzo ya udereva Bodaboda ya awamu ya tatu katika mji mdogo wa makambako mkoani Njombe ambapo amesema kuwa madereva wanatakiwa kutembea na vivuli vya vyeti vyao vya udereva ili kutambua waliosoma na ambao hawajasoma.
Amesema kuwa madereva wengi wa pikipiki wapo barabarani bado hawajapatiwa elimu ya usalama barabarani na kuwa wengine wakifanya shughuli za udereva kwa kutumia reseni walizotafutiwa na ndugu zao.
Mgeni rasimi katika hafla hiyo Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Njombe Lameck Noah kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dk. Rehema Nchimbi amewataka madereva hao kuwacha mbwembe na mikogo wanapo endesha vyombo vyao kwa kuwa wanaweza kusababisha ajali kwa watu wanao tumia barabara na madhara kwao wao.
Hata vivyo Kamanda wa polisi Mkoa wa Njombe, Pudensiana Protas amesema kuwa madereva hao waliopata vyeti, wakawe waalimu kwa madereva wenzao na kuwataka kuhakikisha kuwa wanawashawishi kwenda shule.
Upande wao wahitimu hao wamesema kuwa walikuwa wakiendesha vyombo vya moto kwa uzoefu bila kwenda shule.