Jumapili , 25th Mei , 2014

Serikali ya Tanzania imeshauriwa kuondoa ada katika leseni ya biashara ambayo inaweza kumsababishia mfanyabiashara mdogo kurudi nyuma kimaendeleo.

Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya mapato nchini Tanzania TRA, Rished Bade. Mamlaka yake ndio mkusanyaji mkuu wa kodi, mapato na ushuru wote wa serikali.

Wito huo umetolewa leo jijini Dar es salaam na mwenyekiti wa Taasisi ya wafanyabiashara wadogo nchini VIBINDO Bw. Gastoni Kikuwi wakati alipokuwa akizungumza na East Africa Radio mara baada ya taasisi hiyo kufanya utafiti wa athari za kurejeshwa kwa ada hiyo ambayo hapo awali ilikuwa imeondolewa.

Amesema katika utafiti huo wamegundua kwamba kuendelea kuwepo kwa ada hiyo inaweza kuathiri mfumo mzima wa wafanyabiashara wadogo kutokana na kiwango cha ada hiyo kuwa kikubwa.