Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe.Medard Kalemani.
Wachimbaji hao wamezungumza na katika mkutano kati yao na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe.Medard Kalemani kilichofanyika mjini mpanga na kusema kuwa tatizo hilo linawafanya wachimbaji wengi kushindwa kufaidika na biashara hiyo.
Wachimbaji hali pia inawafanya kukosa soko la nje kutokana na walanguzi wachache kuendelea kuwakandamiza kwa kununua dhahabu zao kwa bei ya kutupa kwa madai hiyo madini hayo yamepunguza thamani nje ya nchi.
Akizungumza na wachimbaji hao Naibu waziri wa Nishati na Madini Dkt. Merdad Kelamani amesema kuwa wachimbaji hao wanapaswa kuzijua sheria za uchimbaji na uuzaji madini hayo ili kuepuka kulipa mirabaha mara mbilimbili.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa wachimbaji wadogo mkoani humo William Mbogo amesema kuwa wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo kutotengewa maeneo maalumu kwa ajili ya wachimbaji wadogo.