Jumatano , 28th Mei , 2014

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo limeendelea na vikao vyake vya bajeti ambapo hoja ya bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imezua mjadala mzito uliojikita katika migogoro ya radhi iliyopo nchini kwa sasa.

Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi nchini Tanzania, Profesa Anna Tibaijuka.

Wakichangia hoja ya wizara hiyo kwa nyakati tofauti, baadhi ya wabunge wameonyesha kutoridhishwa na utendaji wa wizara ya ardhi , hususani katika kutafuta ufumbuzi wa migogoro ya ardhi iliyopo baina ya wananchi na wawekezaji pamoja na ya wakulima na wafugaji.

Nayo Kamati ya Bunge ya Ardhi na Maliasili katika maoni yake kuhusina na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, pamoja na mambo mengine iliibua hoja ya mradi wa mji wa Kigamboni Jijini Dar es Salaam ambao hadi sasa haujulikani ni lini utaanza.