Mwenyekiti wa bodi ya wahariri(TEF) Bw, Absolom Kibanda.
Imeelewa kuwa hali hiyo inatokana na kutekwa na hisia za upande mmoja na kusababisha uchaguzi mkuu kutokuwa wa amani, haki na usalama.
Akiongea wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya uandishi wa habari yaliyoanza leo bagamoyo Mwenyekiti wa bodi ya wahariri (TEF) Bw, Absolom Kibanda amesema waandishi wanapaswa kujua uchaguzi kwa wakati huu utatawaliwa na mambo makubwa ambayo hawajawahi kukutana nayo kutokana na viashiria vingi vilivyojionesha na vinavyoendelea kujionesha.
Aidha amesema waandishi watakuwa watu wa ajabu kama wataandika habari za uchaguzi bila kufanya hadidu za rejea za chaguzi kuu zilizopita, kujua wagombea urais, ubunge na udiwani hata na idadi za majimbo, hivyo umakini mkubwa unatakiwa kwa kipindi hiki huku akisisitiza mafunzo hayo.