Jumanne , 5th Jul , 2016

Mamia ya watu wameandama jana katika mji mkuu Nairobi, Kenya kulaani mauaji ya kiholela kufuatia kuuawa kwa watu watatu wiki iliyopita akiwemo wakili wa kutetea haki za binadamu Willie Mwangi aliyekuwa mkosoaji wa ukiukaji unaofanywa na polisi.

Baadhi ya Wananchi wakiwa wameandamana nchini Kenya

Waandamanaji waliokuwa wamevalia fulana zilizopakwa rangi nyekundu kuashiria damu wanataka uchunguzi ufanywe kuhusu mauaji hayo.

Mwili wa Kimani, mteja wake Josephat Mwenda na dereva Joseph Muiruri ilipatikana Ijumma iliyopita katika mto Ol Donyo Sabuk katika kaunti ya Machakos baada ya watatu hao kuripotiwa kupotea tarehe 23 mwezi Juni walipokuwa wakitoka mahakamani.

Mashirika 34 ya ndani ya Kenya na ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu yamelaani mauaji hayo. Askari watatu wanazuiwa kwa kushukiwa kuhusika na mauaji hayo.