Wa kwanza kutangaza vita ya pili ya dunia afariki

Tuesday , 10th Jan , 2017

Mwandishi wa habari Clare Hollingworth, mkongwe aliyetangaza habari ya kuanza kwa vita ya pili ya dunia amefariki dunia Hong Kong akiwa na umri wa miaka 105.

Clare, hapa alikuwa na miaka 104

Clare Hollingworth alizaliwa katika mji wa Leicester nchini Uingereza mwaka 1911, na ndiye mwandishi wa habari aliyetangaza taarifa ya Ujerumani kuivamia Poland mwezi Agosti mwaka 1939.

Mwandishi huyo aliendelea kuripoti habari huko Vietnam, Algeria na Mashariki ya kati.

Wakati akiibuka na habari hiyo ya kuanza kwa vita ya pili ya Dunia, Bi Hollingworth alikuwa mwandishi kinda wa gazeti la Daily Telegraph.

Kabla ya kuwa mwandishi wa habari alisaidia maelfu ya watu kutoka katika jeshi la Hitler kwa kuwasaidia kupata viza ya Uingereza na ni yeye aliyeyaona majeshi ya Ujerumani yakitanda katika mpaka wa Poland wakati akisafiri kutoka Poland kwenda Ujerumani mwaka 1939.