Jumamosi , 25th Jun , 2016

Ikiwa leo siku ya mwisho kwa vyama vya siasa nchini kuwasilisha nyaraka ya gharama za uchaguzi za mwaka 2015 zoezi hilo limeonekana kusuasua ambapo mpaka kufikia saa sita mchana vyama viwili tuu vilivyojitokeza .

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaa, Mkuu wa Masijala kutoka ofisi ya Msajili Mkuu wa vyama vya siasa nchini Galasia Simbachawene amesema kuwa hadi saa sita mchana vyama viwili ambavyo ni Chama Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Chama cha Alliance For Democratic Change (ADC) ndio vilivyofanikiwa kuwasilisha ripoti yake ambapo imefanya jumla yavyama 5 kati ya vyama 18 vilivyoshiriki uchaguzi mwaka huu.

Vyama vingine ambavyo vilishakabidhi ripoti ya hesabu za gharama za uchaguzi ni pamoja na Chama cha Mapinduzi (CCM), ACT wazalendo na Chama cha Wananchi CUF.

Akizungumza mara baada yakukabiidhi nyaraka hizo Kamishna Mkuu wa chama cha ADC, Don Mnyamani ameimbia EAST Africa Radio kuwa sheria hiyo ni mzuri ambayo inathibiti fedha haramu kutumika katika uchaguzi lakini inawabana watu wasiokuwa na fedha kushiriki katika uchaguzi kutokana na kukwepa kupata fedha haramu na kuomba msajili kufikiria upya sheria hiyo.