Alhamisi , 5th Oct , 2023

Vyama 11 tofauti vya upinzani nchini Zambia vimeungana kulaani  matatizo ya kiuchumi, "umasikini" na "ukosefu wa ajira" wanaosema umeongezeka chini ya Rais Hakainde Hichilema.

Viongozi kutoka vyama hivyo  ambao walifanya mkutano wa pamoja na waandishi wa habari Jumatano  walisema wana wasiwasi mkubwa na waliitisha mkutano wa kitaifa kujadili hali ya nchi.

Katika barua ya wazi kwa Rais Hichilema, waliorodhesha masuala 18, miongoni mwao  bei ya juu sana  ya bidhaa za msingi na  kukamatwa kwa kiholela na unyanyasaji wa mara kwa mara wa wanachama wa upinzani.

Barua hiyo pia ilidai kuwa hatua ya serikali ya kukuza  sera za kimataifa, ushirika, nje na za kizalendo   zimesababisha uharibifu mkubwa kwa uchumi na ustawi wa watu .

Chama cha Kisoshalisti, All People's Congress Party na chama tawala cha zamani cha Patriotic Front, ni miongoni mwa waliotia saini barua hiyo.

Nchi hiyo ya kusini mwa Afrika imekumbwa na mgogoro wa madeni wa miaka mitatu - imekuwa taifa la kwanza la Afrika kushindwa kulipa madeni yake wakati wa janga la Covid.

Licha ya kuwa na utajiri wa shaba, mikopo na viwango vya juu vya riba vimezuia sana uwezo wa Zambia kuwekeza katika mipango muhimu ya kijamii na miundombinu.