
Mfano wa Nyumba
Kutokana na ugumu wa maisha pamoja na gharama kubwa ya ujenzi hasa mijini, wakazi wengi hupendelea kupanga katika nyumba za watu huku wakijipanga katika maisha yao. Kuna vitu vingi vya kuzingatia wakati wa utafutaji nyumba ya kupanga ili uweze kufurahia na kuishi kwa amani mahali husika.
Wachangiaji mbalimbali wametoa maoni yao kwenye kipindi cha funguka kinachoruka kupitia EATV pamoja na ukurasa wa Facebook, ambapo mada ya leo imeuliza "Kitu gani huzingatia kukiangalia cha kwanza ukitaka kupanga nyumba na kwanini ?", na haya hapa ni baadhi ya maoni.
Richard Shaully: wa Mlandizi, nyumba sio pambo bali makazi salama. Maadui wa afya wasiwepo, kisaikolojia pawe tulivu, amani itawale na yote kwa yote mandhari yenye mvuto kwa wageni na mwisho, barabara ifikike kirahisi ili kupata huduma za msingi.
Amina Tarimo: wa Dodoma aisee huwa mimi kabla ya yote naangalia choo, na maji.
Mbaga Charles Kubeja: wa Kishinda, Geita
Kitu cha kuzingatia ukiwa unapanga nyumba cha kwanza utambue usalama uliopo katika mtaa huo pia utambue idadi ya watu walio panga mahali hapo, ila epuka sana kukuta wanawake ambao hawajaolewa kuanzia na watatu tambua na wewe pale utakuwa umefata mambo hayo tu hakuna upangaji tena.
Emmanuel Kipele: chakwanza naangalia kama baba mwenye nyumba anaishi hapo hapo maana bora nikose choo nita kichimba ila sio baba mwenye nyumba na yeye aishi hapo hapo sitaki kabisa, maana utasiki akiishiwa unga kwake utasikia hodi mara anaanza urafiki kwa mkeo mwisho wa siku anatoka na mkeo, tabu hizo sizitaki.
Shamila Manga: masha apa, mimi naangalia choo na wapangaji wezangu waishivyo yaani ustaarabu na usafi nini zamu iko vizuri au maugomvi na nyumba ilivyo hicho cha mwisho kabisa.
Kwa mujibu wa tafiti nyingi zisizo rasmi zinaonesha kuwa karibia nusu ya wakazi wa Dar es Salaam wanaishi katika nyumba za kupanga, kwahiyo vigezo hivi vinaweza kuwa msaada kwa wengi ambao wako katika mchakato wa kutafuta sehemu za kupanga.