Askari wa Jeshi la Polisi Kigoma wakionesha vipande vya meno ya Tembo vilivyokamatwa
Vipande 11 vya meno ya tembo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 10 vimekamatwa na polisi wakati vikisafirishwa kutoka wilayani Mpanda mkoani Katavi kwenda mkoani kigoma.
Kamanda wa polisi mkoa wa kigoma, Frasser Kashai amesema, watuhumiwa kadhaa wanahojiwa kuhusiana na usafirishaji wa nyara hizo kabla ya kufikishwa mahakamani .
Amesema kukamatwa kwa pembe hizo za Tembo kunatokana na taarifa za raia wema ambapo amesema jeshi hilo limeongeza doria na upekuzi ili kudhibiti wimbi la ujangili na usafirishaji wa mazao ya maliasili.
Kwa upande wake afisa ulinzi wa wanyamapori katika hifadhi ya taifa ya Gombe mkoani Kigoma Dominick Tarimo amewataka watanzania kukabiliana na wimbi la ujangili ambalo linatishia kutoweka kwa baadhi ya wanyama na hasa Tembo ambao wamekuwa wakiuliwa na majangili