Jumanne , 27th Jan , 2015

Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA mkoani Arusha kimesema kitaendelea kuungana na wananchi kukemea na kukabiliana na viongozi wanaowakejeli na kuwakatisha tamaa watanzania wanaotaka kuwekeza kwenye miradi mikubwa ukiwemo wa gesi na mafuta.

Katibu wa CHADEMA Arusha Kalsto Lazaro

Kimesema kuendelea kuwafumbia macho viongozi wa aina hiyo ni kuendekeza umaskini.

Akizungumzia mabadiliko yaliyofanywa katika Wizara ya Nishati na Madini katibu wa chama hicho Bw Kalsto Lazaro amemtahadharisha waziri Geoge Simbachawene aliyeteuliwa kuchukua nafasi ya Prof Muhongo aliyejizulu kuacha kuendelea kuwakatisha watanzania tamaa badala yake awape moyo na kuwasaidia kufikia ndoto zao.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wamesema mtu yeyote anayekatisha wenzake tamaa badala ya kuwapa moyo ni ishara ya kutosha kuwa amepoteza sifa ya kuwa kiongozi na pia uwezo wake wa kuleta mabadiliko ni mdogo kwani hakuna lisilowezekana.