Ijumaa , 24th Oct , 2025

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamekubaliana kuisaidia Ukraine kifedha katika kipindi kingine cha miaka miwili.

Lakini hata hivyo wameshindwa kutoa mamilioni ya fedha za Urusi zilizozuiwa ili kutoa ufadhili wa ulinzi wa nchi hiyo
Katika mkutano wao wa jana viongozi hao waliahirisha uamuzi wao wa kutumia kiasi ya Euro bilioni 140 za mali ya Urusi zinazoshikiliwa nchini Ubelgiji hadi hapo Desemba.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameeleza mkutano huo wa Ubelgiji kwamba hatua hiyo italeta matokeo chanya.

Mkutano huo wa Brussels ulifanyika jana wakati kukitarajiwa kufanyika mkutano mwingine huko London ambako Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer anatarajiwa kuwahimiza viongozi wa Ulaya kuongeza kupeleka vifaa vya kijeshi nchini Ukraine.