Sheikh Mkuu na mufti wa Tanzania Issa bin Shabaan Simba akipeana mikono na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.
Shekhe Shaaban ametoa kauli hiyo leo mjini Dodoma wakati akizungumza na East Afrika Radio kuhusiana na kauli aliyoitoa Rais Kikwete ya kuwataka viongozi wa dini nchini kutowaruhusu wanasiasa kufanya siasa zao kwenye nyumba za ibada.
Amesema Rais ni kiongozi mkubwa wa serikali kwa hiyo kauli yake ni lazima izingatiwe ili kuliepusha taifa na vita ya udini ambayo mara zote huwa haina mshindi.
Kwa upande wake Askofu wa Kanisa la Pentecoste Bible Fellowshi in Tanzania, Jafeth Mapogo amesema kuwa kauli ya Rais ni ya kuzingatiwa ili kuepusha vita ya udini kwani ndani ya nyumba za ibada kuna wanachama wa vyama mbalimbali vya siasa hivyo kuruhusu siasa ndani ya nyumba za ibada ni kuhatarisha amani ya nchi.