Viongozi wa Dini ya kikristo nchini wameliomba jeshi la polisi kuimarisha ulinzi katika makanisa ili kuepusha matukio mbalimbali ya kikatili yanayojitokeza mara kwa mara ya kuchomwa kwa makanisa na kuuwawa kwa viongozi wa dini.
Wakiongea na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Kagera viongozi wa dini mbalimbali za kikristo wakiwemo mapadre na wachungaji wamelitaka jeshi la polisi nchin kuimarisha ulinzi katika makanisa ili kunusuru matukio mbalimbali ya kikatili ambayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara hapa nchini ikiwemo kuchomwa kwa makanisa na hata kuuawa kwa viongozi wa dini, ambapo wameongeza kuwa jeshi la polisi lisijihusishe kabisa na masuala ya siasa badala yake lifanye kazi kwa uadilifu ili kulinda amani na utulivu uliopo nchi.
Akijibu malamiko hayo kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Kagera Henri Mwaibambe, amesema viogozi wa dini ni moja ya chombo ambacho kinajitahidi katika kudumisha amani ya nchini ambapo amesikitishwa na vitendo vinavyojitokeza makanisani ikiwemo tukio lililojitokeza hivi karibuni hapa mkoani Kagera la kuuwa kwa mtu mmoja aliyekuwa mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Kagaemu ambaye aliuawa kikatili akiwa anafanya maombi kanisani na kwamba jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi na litahakikisha linaimarisha ulinzi katika maeneo ya makanisa.