Jumanne , 1st Apr , 2014

Wakazi wa vijiji sita wilayani Kilindi mkoani Tanga nchini Tanzania wameathirika na mvua za masika zinazoendelea kunyesha kufuatia kingo za bwawa kubwa mkoani humo kusombwa na maji na kusababisha mafuriko katika baadhi ya vijiji hivyo.

Afisa Mtendaji wa Kata ya Mkindi Bw. Lazaro Kidege amesema kama hazitafanyika jitihada za haraka kudhibiti tatizo hilo itakapofika kipindi cha kiangazi jamii ya wakazi wake ambao wengi wao ni wafugaji na wakulima watahama vijiji vyao.

Mmoja kati ya akina mama wafugaji wamesema kwa sababu wengi wao ni tegemezi athahari zitakazojitokeza ni kubwa kwa kuwa akina baba watakapohama watakaothirika zaidi ni akina mama na watoto hasa wale wanaosoma, ambao watalazimika kuacha shule.