Mkuu wa wilaya ya Chunya Deodatusi Kinawiro
Mhandisi wa maji wa halmashauri ya wilaya hiyo mhandisi Ndele Mengo amevitaja vijiji hivyo kuwa ni Lupa Market Magamba, Sangawana, Mtanila, Matwiga, Mwiji, Luwalanje, Totoe, na Galula.
Amesema kuwa serikali itahakikisha kuwa ifikapo mwaka 2016, wakazi wa vijiji hivyo watapatiwa huduma ya maji safi na salama na kwamba kwa sasa inakamilisha miradi ya maji katika vijiji vya Namkukwe, Udinde, Mwambani, Mbuyuni na Mkola.
Hata hivyo amewataka wananchi kuchangia fedha za kuendesha miradi ya maji kwenye maeneo yao pindi ikihitajika ili kuharakisha kuwasogezea huduma hiyo muhimu.