Wajasiliamali wa viatu
Imefahamika kwamba Vijana wengi nchini Tanzania wanashindwa kufanya biashara kwa kukosa ujasili wa kudhubutu.
Akizungumza na vijana wanaojihusisha na ujasiliamali Mkurugenzi wa Asasi ya kuelimisha na kuwaendeleza vijana Tanzania hasa katika masuala ya uchumi na ujasiliamali Bwana Peter Masika amewataka vijana kuwa na mila yakugeuza mawazo yao kuwa mtaji.
Kwa upande wake muwakilishi wa taasisi za fedha zilizodhamini mafunzo hayo Bi Irene Peter amezitaka taasisi zingine nchini kuhakikisha wanawasaidia vijana kuwawezesha kimitaji kwa kuwapa mikoplo ya bei nafuu.
Nao washiriki wa mafunzo hayo wamewaasa vijana wenzao kuachana na makundi yasiyo na faida na wajiunge katika kujenga uchumi wa nchi.




