Jumatano , 4th Jun , 2014

Vijana wanaomaliza elimu ya juu nchini Tanzania wameshauriwa kuwa na mbinu mbadala ambazo zitawezesha kujiajiri badala ya kukaa vijiweni na kuisubiri serikali kuwapatia ajira jambo ambalo limeelezwa kupita na wakati.

Katibu mkuu wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel (kushoto). Ofisi yake ina jukumu la kuandaa mazingira mazuri kwa vijana wabuni ajira.

Ushauri huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mtaalam Elekezi kutoka Taasis ya Vijana ya TYC, Dkt. Rashid Msindo wakati wa mkutano wa pamoja wa vijana kutoka maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam ili kujadili fursa za ajira kwa vijana.

Dkt. Mshindo amesema vijana wana wajibu wa kuangalia fursa zilizopo ili kuona namna watakavyojiajiri kuliko kumaliza elimu ya juu na kusubiri ajira kutoka serikalini.