Jumapili , 27th Mar , 2016

Katika kuhakikisha vijana wanajiajiri na kuanza kujiingizia kipato wao wenyewe katika vikundi mbalimbali Chuo cha Maendeleo ya Jamii mkoa Njombe kimeanza kutoa elimu ya utengenezaji wa matofari rahisi kwaajili ya vijana hao kuanza kujiajiri.

Vijana wakiwa katika mafunzo ya ufyatuaji matofali.

Akizungumza baada ya kumaliza mafunzo ya siku tatu ya utengenezaji wa tofari hizo kiongozi wa kikundi cha Tulipamwambu, Betram Ngimbuzi amesema kuwa wamepata mafunzo ya utengezezaji wa tofari rahisi ambazo ni imara.

Amesema kuwa mafunzo hayo yametolewa chini ya sheria ya makazi bora namba 30 ya mwaka 1997 ambayo inamtaka kila mwananchi kuwa na makazi bora.

Aidha baadi ya wana vikundi walioshiriki mafunzo hayo kutoka katika vikundi vitatu vya mkoani Njombe vya Tulipamwabu, Njombe Imagination na vijana wa chuo cha maendeleo wamesema kuwa mafunzo hayo yanawafanya wao kujiari na kuwasaidia watanzania kujenga nyumba imara kwa bei nafuu.