
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kinondoni shamba Vicent Mhepwa.
Akiongea na EATV leo Mhepwa amesema mara baada ya kuvuta aina hiyo ya ulevi vijana hao wanalewa na kulala pamoja na kufanya vitu ambavyo haviendani kimaadili katika mtaa huo.
Mhepwa amesema kuwa kwa kushirikiana na jeshi la polisi kuna wakati waliweza kudhibiti kwa kiasi kikubwa matumizi ya madawa za kulevya kwa vijana wa mtaa huo lakini kwa sasa wamebuni mbinu mpya ambayo pia wanalifanyia kazi suala hilo ili kudhibiti aina hiyo ya dawa za kulevya.
“Kipindi ambacho kumekuwepo na wimbi kubwa la matumizi ya bangi na dawa za kulevya tulifanikiwa kuwakamata vijana hao kwa kushirikiana na jeshi la polisi na tatizo hilo likapungua lakini sasa wamekuja na mbinu mpya ya kuchanganya dawa za usingizi na moyo wa betri” amesema mwenyekiti huyo