Jumatano , 17th Jul , 2024

Watafiti wa afya nchini wameeleza kuwa kwa sasa changamoto ya lishe duni imekuwa kichocheo cha athari za matatizo matatizo ya afya ya akili, licha ya maeneo mengi nchini kuwa na uhakika wa upatikanaji wa vyakula vya lishe bora. 

Amani Tinkasimile Mtafiti wa masuala ya afya hasa kwa vijana na wanawake wajawazito, kutoka Africa Academy for public Health.

EATV imefanya mahojiano Maalum na Amani Tinkasimile Mtafiti wa masuala ya afya hasa kwa vijana na wanawake wajawazito, kutoka Africa Academy for public Health, ametueleza kuwa kwa sasa kundi la vijana limekuwa hatarini kwa kukosa lishe bora, kwani kati ya vijana kumi (10), watano (5) wanauzito uliopungua huku 7 kati ya 1000 wanauzito uliokithiri. 

Given Sam ambaye pia ni mtafiti na balozi wa afya ya akili, anakiri kuwa matokeo ya ongezeko la changamoto za afya ya akili kwa kiasi kikubwa yanachochewa na watu kutopata mlo kamili.

Wadau wanaomba serikali kuweka nguvu kubwa katika kuruhusu upatikanaji wa taarifa za taasisi zake kwa watafiti, sambamba na kuongeza juhudi za wananchi kufikiwa na taarifa za matokeo ya tafiti.