
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema hayo katika ujumbe wake wa siku ya kimataifa ya kujua kusoma na kuandika hii leo akisema kuwa hivi sasa zaidi ya watu milioni 750 duniani kote ni wajinga wa kutokujua kusoma na kuandika.
Kati yao hao milioni 115 ni vijana na hivyo kuwa ni kikwazo katika kufanikisha ajenda 2030 ambayo kujua kusoma na kuandika ndiyo kitovu chake.
Bw. Ban Ki-Moon amesema vikwazo hivyo kwa maendeleo endelevu vinaweza kuondolewa kwa kutunga sera sahihi zinazopatiwa kichochea na rasilimali za kutosha.
Amesema ni lazima kuhakikisha watoto ambao hawako shuleni wanapata fursa ya kujifunza, sanjari na kuboresha elimu inayotolewa na kuendeleza elimu ya watu wazima.