Hali ilivyokuwa
Akizungumzia zoezi hilo Afisa Uhusiano wa RAHCO Bi. Catherine Moshi amesema zaidi ya nyumba 200 katika maeneo ya Stesheni hadi Pugu ambazo zimejengwa ndani ya usawa huo zitabomolewa ili kupisha ujenzi kwa kiwango cha Standard Gauge.
Amesema tayari serikali ilishatoa muda kwa wananchi kuondoka katika eneo hilo lakini cha kushangaza ni kwamba mpaka leo wanakwenda kubomoa bado wamekuwepo licha ya kutangaziwa kuondoka.
Bi. Catherine Moshi
Wananchi waliobomolewa wakiwemo wakina mama wamepoteza fahamu na wengine kuondolewa kwa nguvu na polisi kutokana na kugoma kutoka ndani ya nyumba hizo, huku mkazi mmoja aliyegoma kutoka ndani ya nyumba, akitaka afie ndani ya nyumba yake iliyokuwa ikibomolewa, kabla ya askari kwenda kumtoa kwa nguvu.
Tazama video......

