Alhamisi , 11th Mei , 2017

Hosptali ya Taifa Muhimbili imekiri kuwepo kwa uhaba wa watumishi na kuandika barua ya dharura kwa ajili ya kuomba watumishi wapya kuziba pengo la kuondolewa kwa watumishi 134 waliobainika kugushi vyeti vya na kusimamishwa kazi.

Msemaji wa hospitali ya Muhimbili, Bwana Eligaesha amesema kuwa pamoja na kwamba wana uhitaji wana madaktari, kuondolewa kwa watumishi wenye vyeti feki lakini haujaathiri utendaji kazi na kwamba huduma zinaendelea kutolewa kama kawaida na kuongeza kwamba  sasa Hosptali inaendelea na maboresho ya miundombinu na majengo ili kuhakikisha kuwa wanafikia lengo la kutoa huduma bora na kukidhi mahitaji ya wananchi.

Watumishi walioondolewa ni pamoja na madaktari 2, wauguzi 70, kurugenzi ya tiba watu 20, Tiba Shirikishi 14 na nafasi zingine zilizoguswa ni pamoja na wataalamu wa maabara, wafamasia, idara ya kumbukumbu na wahudumu wa afya 19.

Mtazame hapa chini Msemaji wa Hospitali ya Muhimbili.