
Hali hii ya ongezeko inatajwa kufuatia uzinduzi wa filamu ya Royal tour ikielezwa na katibu mkuu Wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji Prof Godius Kyaharara kuwa sekta ya hotel Kwa mkoa wa Dar es Salaam wageni wameongezeka Kwa kipimo Cha 280 huku Arusha wakiongezeka Kwa kipimo Cha 340 upande wa hotel.
Kiashiria kingine kimetajwa kuwa kuongezeka Kwa miruko ya ndege, ongezeko la ndege zinazokuja ndani akibainisha Kila sekta Iko na vipimo vyake katika kujua idadi hiyo.
Kwa upande wao wachumi katika sekta hiyo wameiomba serikali kuweka vipimo vitakavyoweka tathimini Kwa Viongozi wenye dhamana na uwekezaji Ili kuona kama kasi waliyonayo inaridhisha