Ijumaa , 1st Jan , 2016

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Gallawa amewataka wafugaji mkoani humo kuuza mifugo yao ili kuweza kukabiliana na tatizo la njaa linaloukabili mkoa huo kwa sasa.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Luteni Chiku Gallawa

Gallawa ametoa wito huo wakati akizungumza na East Africa Radio kwa njia ya simu, kuhusiana na hatua zinazochukuliwa na serikali ya mkoa wa Dodoma katika kukabiliana na tatizo la njaa lililozikumba baadhi ya Wilaya mkoani humo.

Aidha mkuu huyo anaeleza kuwa kuna tani za chakula ambazo zimetengwa kwa ajili ya kuwanusuru wananchi wanaokabiliwa na tatizo hilo.

Baadhi ya wilaya za mkoa wa Dodoma ikiwemo Kondoa, Bahi na Mpwapwa zinakabiliwa na baa la njaa hali iliyowapelekea kuwalazimu wakazi hao kula matunda pori ili kuweza kunusuru uhai wao.