Jumatatu , 9th Jun , 2014

Ukosefu wa uwazi na uwajibikaji miongoni mwa viongozi wa serikali ya Tanzania kumeelezwa kunachangia kwa kiasi kikubwa kutofanikiwa kwa shughuli za Maendeleo ya Jamii nchini.

Mhadhiri wa chuo kikuu cha Mtakatifu Augustine, Profesa Mwesiga Baregu.

Hayo yameelezwa na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mt. Augustino, Prof. Mwesiga Baregu wakati wa mkutano wa pamoja na asasi na mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali wenye lengo la kujadili namna ya kuleta chachu ya maendeleo kwa viongozi wa serikali.

Kwa upande wake, Waziri wa nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Utawala Bora, Kapteni Mstaafu George Mkuchika amesema asasi za kiraia zina mchango mkubwa katika kuhamasisha uwajibikaji miongoni mwa viongozi wa serikali.