
Majaliwa amewahakikishia wawekezaji hao kuwa Serikali ya Tanzania ipo tayari kwa uwekezaji wao na itawawezesha kuwekeza mitaji yao ukiwa ni mkakati wa uendelezaji wa madini ya kimkakati nchini Tanzania
“Sisi tuna madini na ninyi ndugu zetu Wakorea mna mitaji, twende tuunganishe nguvu kwa manufaa ya nchi zote,ninapenda kuwahakikishia kuwa nchi yetu ni salama na Mheshimiwa Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan anafanya kila linalowezekana kuboresha mazingira ya kufanya biashara na uwekezaji nchini”Amesema Kassim Majaliwa.
Kwa upande wake, Mjumbe Maalumu wa Rais wa Korea ambaye ndiye kiongozi wa ujumbe huo kutoka Korea Kusini Yoon Sang Jick ameishukuru Serikali ya Tanzania na kwamba wataendelea kushirikiana nayo kuhakikisha malengo ya uwekezaji yanafanikiwa.
Naye, Waziri wa Madini Anthony Mavunde ameishukuru Korea Kusini kwa kuichagua Tanzania na kufanya mazungumzo kuhusu uwekezaji katika sekta ya madini. Ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji kutoka nchini humo waje wawekeze Tanzania.