Mabehewa ya treni
Amesema hayo mara baada ya kutembelea kampuni hizo zilizopo katika mji wa Changwon, Korea ya Kusini, zilizoingia mkataba na serikali ya Tanzania, wa kutengeneza mabehewa 59 na vichwa vya treni 17 pamoja treni za mwendokasi (Electric Multiple Unit) 10.
"Kwa kampuni zote mbili maendeleo ni mazuri kwa hatua iliyofikiwa na wametueleza kuwa wanatarajia kukamilisha utengenezaji wa mabehewa na vichwa vya treni kama ilivyoainishwa katika makubaliano, na kwa kweli tuliyoyaona yako katika hali nzuri," amesema Amina.
Aidha, alitumia nafasi hiyo kutoa maelekezo kwa sekta husika kuhakikisha kuwa inatoa mafunzo kwa watakaohusika na kuendesha, kuhudumia treni hizo wanajengewa uwezo ili ziweze kudumu kwa muda mrefu na kutoa huduma bora kwa uendelevu.
Ujumbe wa Tanzania ulikuwa Busan Korea ya Kusini kuhudhuria mkutano wa saba wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea Kusini na Nchi za Afrika (KOAFEC), Mjini Busan, Jamhuri ya Korea Kusini ambapo Tanzania iliungana na nchi nyingine za Afrika katika mkutano huo.