Jumatatu , 26th Jun , 2023

Watawala wa kijeshi wa nchi hiyo na mataifa yenye nguvu ya kikanda wamesema uchaguzi huo utapelekea uchaguzi wa Februari mwakani na kisha kurejea kwa utawala wa kiraia.

Mkuu wa tume ya uchaguzi,Moustapha Cisse, alitangaza kuwa Idadi ya wapiga kura milioni 8.4 waliojiandikisha ilikuwa chini ya asilimia 40.

Nchi hiyo imeshuhudia mapinduzi mawili ya kijeshi tangu Agosti 2020, wakati Rais Ibrahim Boubacar Keïta alipopinduliwa.

Kiongozi wa Junta na Rais wa mpito Assimi Goïta alisema katika hotuba yake kwamba ameshawishika kwamba kura hii ya maoni inafungua njia kwa Mali mpya, yenye nguvu, yenye ufanisi na inayoibuka, lakini zaidi ya yote Mali katika huduma ya ustawi wa watu.

Kabla ya kura ya maoni kulikuwa na wasiwasi kwamba katiba mpya itatoa mamlaka makubwa kwa rais, ambaye sasa atakuwa na haki ya kuajiri na kumfukuza waziri mkuu na mawaziri.

Chini ya mabadiliko hayo, bunge la pili linatarajiwa kuundwa ili kuimarisha uwakilishi mpana wa kisiasa