Alhamisi , 18th Mei , 2023

Jeshi la Polisi mkoani Tabora linaendelea na uchunguzi kufuatia utata wa vifo vya watoto mapacha  ambao walizaliwa njiti katika kituo cha afya Kaliua kilichopo mkoani humo ambapo mtoto mmoja alikutwa ameondolewa ngozi ya  paji la uso na kuharibiwa jicho moja la upande wa kulia.

Kushoto ni mmoja wa kichanga aliyechunwa ngozi usoni na kulia ni Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Tabora ACP  Costantine Mbogambi.

Taarifa hiyo imetolewa hii leo Mei 18, 2023, na Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Tabora ACP  Costantine Mbogambi.

Amesema watoto hao baada ya kufariki dunia  wakiwa katika kituo cha afya wanafamilia walikabidhiwa miili ya watoto hao ambapo kabla ya kuwazika mmoja alionekana akiwa  amechunwa ngozi ya paji la uso pamoja na kuharibiwa jicho moja la upande wa kulia .

Mpaka sasa miili ya watoto hao bado imehifadhiwa katika hospitali ya wilaya  ya Urambo baada  ya wanafamilia  kukataa kufanya maziko  mpaka  uchunguzi  wa mzingira ya kifo cha watoto hao utakapokamilika.