Jumanne , 25th Mei , 2021

Mbunge wa Hai Mhe. Saashisha Mafuwe amesema vyama vya ushirikia nchini ni mmoja ya kero kubwa iliyosababisha umaskini katika jimbo la Hai Mkoani Kilimanjaro kwani asilimia 78 ya mashamba yapo chini ya ushirika.

Mbunge wa Hai Mhe. Saashisha Mafuwe

Mhe. Saashisha amesema hayo bungeni Dodoma wakati akichangia hoja katika bajeti ya Wizara ya Kilimo ambapo amesema nia ya kuanzishwa kwa vyama vya ushirika ilikuwa ni kwa ajili ya kubadilisha maisha ya Watanzania tofauti na hali ilivyo kwa sasa.

“Ushirika si ushirika tena Mhe. Waziri na wewe unajua, watu wachache ndio wanaedesha hawa wanaingia mikataba ya hovyo duniani hujapata ona, kule hai moja ya kero iliyosababisha umasikini ni vyama hivi vya ushirika, sisi ushirika wetu kule unachukua kijiji kizima wanakuwa sehemu ya ushirika, asilimi 78 ya mashamba yetu yapo chini ya ushirika,“ amesema Mhe. Saashisha.

Pia Mbunge huyo wa Hai amesema kuwa vyama vya ushirika ndio chanzo cha kilimo nchini kutokuendelea huku akidai kuwa uwepo wa wizi katika vyama hivyo.

"Katika maeneo yana majizi ni kwenye ushirika, hao ndio wanaoturudisha nyuma hao ndio wanaofanya kilimo nchi hii kisiendelee, mimi kuna siku mtaniweka ndani kwenye mambo haya ya ushirika maana kama mashamba tunayaona si tunagawana tu," amesema Mbunge huyo wa Hai.