
Meneja leseni kwa usafiri wa barabara wa Sumatra Bw. Leo Ngowi amesema hayo katika mahojiano na East Africa Radio ambapo amesema tatizo lililopo hivi sasa ni kwa wasafiri wa kati ya Dar es Salaam na mji wa Bagamoyo kutokana na kutokamilika kwa ukarabati wa kipande cha barabara kwenye daraja la mto Mpiji ambalo nalo liliathirika na mafuriko.
Hata hivyo baadhi ya wasafirishaji na wauzaji wa jumla jumla wa bidhaa za vyakula, wametahadharisha juu ya uwezekano wa kuongezeka bei za bidhaa kutokana na kasi ndogo ya uingiaji wa malori ya mizigo yanayotumia barabara ya Dar es Salaam-Chalinze kama anavyoeleza mfanyabiashara soko la Urafiki Bw. Stamili Salum Mohammed.