Akizungumza mara baada ya kukagua kazi ya upanuzi wa uwanja huo unaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 11.8, Prof. Mbarawa amemtaka Mkandarasi huyo kuhakikisha kuwa ujenzi wa uwanja huo unafanyika kwa kuzingatia viwango vilivyokubalika katika mkataba na kuukabidhi kwa wakati.
“Hakikisheni upanuzi huu unakamilika kwa wakati ili kuupa hadhi inayostahili uwanja wa ndege wa Dodoma, hasa mkizingatia umuhimu wake kitaifa," alisema Prof. Mbarawa.
Naye Mkandarasi anaejenga uwanja huo amemhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa atahakikisha ujenzi wake unazingatia viwango na kuukabidhi katika muda uliokubalika kimkataba.
