Jumapili , 18th Mei , 2014

UNDP imejipanga kusaidia upandaji wa miti Wilayani iringia kwa kutoa mbegu zaidi ya Milion 3 kwa vikundi vya uhifadhi wa mazingira.

Baadhi ya mbegu za miti zilizotolewa na UNDP

Shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, kwa kushirikiana na shirika la kujenga uelewa na mtazamo katika uhifadhi (BMF), limetoa mbegu za miti zaidi ya mil. 3 kwa vikundi vya uhifadhi mazingira katika vijiji 19 vya wilaya ya Iringa kwa ajili ya kupunguza uharibifu wa mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Mratibu wa shirika la BMF ambalo linatekeleza mradi huo kwa kushirikina na Jumuiya za wananchi wanaotumia maji katika bonde la mto Lyandembela Bwana Heri Kayuki amesema miti hiyo inalenga kusaidia kuongeza kipato kwa wananchi ikiwa ni njia mbadala ya kupunguza kasi ya ukataji miti na kuwa kama shughuli za wananchi kujipatia kipato ili wasiharibu mazingira:

Baadhi ya wananchi wamesema kuwa mradi huo unaweza kuzalisha ajira na kupunguza uhamiaji wa vijana kwenda mijini bila matumaini, hasa wakati huu ambapo wilayani humo kuna makundi ya vijana wasichana kwa wavulana wanakimbia mazingira magumu ya vijijini wakiwa na matarajio ya kupata kazi mjini bila kuwa na elimu na hata ujuzi wowote wa kuwawezesha kupata vibarua:

Mradi huo unalenga kuchangia utekelezaji wa programu ya taifa ya usimamizi wa rasilimali za misitu na maji kwa madhumuni ya kuboresha maisha ya wananchi, na kuwaongezea kipato kwa kuwashirikisha katika usimamizi na uhifadhi endelevu wa rasilimali hizo.