Katibu Mkuu wa Wizara ya mipango nchini Kenya Saitoti Torome
Katibu Mkuu wa Wizara ya mipango nchini Kenya Saitoti Torome amesema UNDP imesaidia tafiti za hali ya umaskini ambazo zimewezesha kuelekeza fedha maeneo yenye uhitaji zaidi akitaja fedha za mfuko wa maendeleo jimboni, CDF.
Bw. Saitoti amesema sambamba na hilo amewaeleza washiriki utekelezaji wa awamu ya pili ya dira ya maendeleo 2030 ya Kenya, MTP TWO ikiwemo kuwawezesha kina mama na vijana ili waanzishe miradi midogo midogo ya kuwainua kiuchumi.
Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Mipango ameongeza kuwa lengo la mipango hiyo ni kuweza kuondosha kabisa hali ya umasikini nchini humo na hivyo kuifanya Kenya nchini yenye uchumi mkubwa mpaka kufikia 2030.