Jumamosi , 20th Feb , 2016

Wizara ya Maji na Umwagiliaji imeanza kuchukua hatua za kukabiliana na uchafuzi pamoja na uharibifu wa mazingira unaotokana na shughuli za kibinadamu.

Mto Ruvu ukiwa umefurika maji

Wizara ya Maji na Umwagiliaji nchini Tanzania kwa kushirikiana na shirika la maendeleo la umoja wa mataifa UNDP wameanza kuchukua hatua za kukabiliana na uchafuzi pamoja na uharibifu wa mazingira unaotokana na shughuli za kibinadamu ikiwemo mifugo katika vyanzo vikubwa vya maji vya Mto Ruvu na mto Zigi.

Naibu katibu mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Emmanuel Kalobelo amesema iwapo serikali haitachukua hatua za haraka kuzuia uharibifu huo maji katika mito hiyo yataendelea kupungua licha ya kwamba ndio vyanzo vikubwa vya maji katika maeneo mengi ya nchi.

Naye mkuu wa kitengo cha mazingira kutoka shirika la maendeleo la umoja wa mataifa UNDP Bi. Getrude Lyatuu ameeleza namna shirika hilo lilivyoamua kuanza kusimamia mito hiyo miwili ili isiendelee kuharibiwa.