
Bilionea Bill Gates na mkewe Melinda Gates
Wawili hao wametumia akaunti ya twitter kuandika kuwa baada ya kufikiria sana na kufanyia kazi mno uhusiano wao, wamefikia uamuzi wa kuvunja ndoa yao.
Wawili hao raia wa Marekani walikutana kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 1980 wakati Melinda alipojiunga kampuni ya Bill ya Microsoft.
Wanandoa hao mabilionea wamejaliwa kupata watoto watatu na kwa pamoja wanaongoza taasisi yao ya Bill & Melinda Gates Foundation.
Taasisi hiyo imetumia mabilioni ya fedha kukabiliana maradhi ya kuambukiza na kuhimiza chanjo kwa watoto.