Ijumaa , 9th Oct , 2015

Umoja wa Mataifa UN umeitaka nchi ya Tanzania kuhakikisha kuwa Uchaguzi unafanyika kwa amani ili kusaidia kutekeleza kiurahisi malengo mapya endelevu SDG's.

Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa(UN) na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) hapa nchini, Alvaro Rodriguez

Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na Mratibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa hapa Nchini Alvaro Rodriguez wakati akiongea na waandishi wa habari na kuongeza kuwa nchi ikikosa amani pamoja na utulivu wa kisiasa ni vigumu nchi hiyo kuweza kufikia maendeleo endelevu.

Alvaro ameongeza kuwa lengo no.16 la linasisitiza kulinda na kudumisha amani duniani ili kufikia malengo hayo mapya 17 baada ya kuisha kwa malengo 20 ya milenia

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya nje Balozi Simba Yahaya amesema kuwa amani ni nguzo muhimu sana katika maendeleo ya nchi yoyote na kuonya kuwa Tanzania lazima ijifunze kwa nchi zilizofanikiwa lakini baada ya kuingia katika vita zimerudi nyuma kimaendeleo na kuwa masikini.