Jumatano , 10th Feb , 2016

Serikali imeiagiza MKURABITA kuhakikisha wananchi wanapata haki miliki za kimila za ardhi kupitia ofisi za TAMISEMI.

Serikali ya Tanzania imeitaka ofisi ya Mpango wa Taifa wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge – MKURABITA, kuhakikisha wananchi wanapata hati miliki za kimila kupitia ofisi za TAMISEMI, kwa ajili ya utekelezaji wa matumizi bora ya ardhi hasa yale yanayolenga kuongeza kipato cha kila siku cha kila kaya pamoja na pato la taifa.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumisi na Utawala Bora Bi. Angela Kairuki, ametoa agizo hilo jijini Dar es salaam leo wakati alipokutana na viongozi wa MKURABITA, kwa lengo la kupanga na kuangalia namna nzuri ya kupunguza matatizo yatokanayo na ukosefu wa hati miliki hasa maeneo ya vijijini.

Waziri Kairuki amesema hadi sasa ni asilimia 10 pekee ya ardhi hasa ile ya maeneo ya vijijini nchini ndiyo imeandaliwa kwa ajili ya matumizi bora ya ardhi, huku kukiwa hakuna mipango mizuri kwa ajili ya asilimia 90 ya ardhi iliyobakia, sababu kuu ikitajwa kuwa ni kutokana na ucheleweshwaji wa hati miliki hizo.

Kwa upande wake mkurugenzi wa MKURABITA nchini Bi Seraphia Mgembe amesema kuwa tayari ofisi yake imeanza kushughulikia matatizo ya migogoro hiyo kwa kuwajengea uwezo viongozi kwa ajili ya urasimishaji vijijini...