Jumatano , 12th Jul , 2023

Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda, amesema licha ya Tanzania kuingia katika uchumi wa kati lakini bado hali ya umaskini imekuwa tishio kwa kuwakabili wananchi hususani wale wanaoishi maeneo ya vijijini.

Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda

Pinda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la kumshauri Rais kuhusu utekelezaji wa masuala ya kilimo na chakula amesema hayo jijini Dodoma baada ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi kuzindua mkakati wa miaka mitano wa kuleta mabadiliko katika kilimo chini ya shirika la ukuaji endelevu wa mifumo ya chakula barani Afrika (AGRA).

Waziri Mkuu huyo mstaafu amesema mabadiliko hayo yanatakiwa kuwatoa wakulima katika hali ya umaskini waliyonayo ikiwamo kutumia teknolojia ya kisasa kwenye uzalishaji.

Awali akizindua mkakati huo waziri wa mifugo na uvuvi ABDALLAH ULEGA amesema mkakati huo wenye kugusa maeneo manne muhimu utaleta matokeo chanya kwa taifa.