Alhamisi , 14th Apr , 2016

Ukosefu wa maabara za kutosha za Utambuzi wa Maandishi umedaiwa kuchangia ucheleweshwaji wa kesi zinazoendeshwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU).

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Kamishna Valentino Mlowola

Mkuu wa Taasisi hiyo mkaoni Manyara, Mugasa Mugasa, amesema kuwa kuna maabara moja tu ya nanma hiyo inayomilikiwa na Jeshi la Polisi nchini na hivyo kufanya suala la utambuzi wa Nyaraka zinazodaiwa kughushiwa kuchelewa kufanyiwa kazi.

Bw. Mugasa amesema kuwa katika kipindi hiki taasisi yake imepokea malalamiko 93 na kufanikiwa kufungua kesi mpya 2 na kuna kesi 21 zinazoendelea Mahakamani huku tatizo kuu ikiwa ni maabara za utambuzi wa maandishi.

Amesema kuwa tatizo hilo linasababisha kesi kuchukua hadi mwaka mmoja hadi miaka miwili kutokana na maabara hiyo kuzidiwa uwezo kutokana na kuhudumia uchunguzi unatoka wilayani na mikoa tofauti nchini.

Aidha, licha ya kutoa wito kwa serikali kuongeza mashine hizo amesema kuwa taasisi hiyo imeendelea kutoa elimu kwa umma ili waweze kutoa ushirikiano katika keshi za rushwa ambapo wananchi wengi wameonekana hawana uelewa juu ya kesi hizo.

Sauti ya Mkuu wa Taasisi hiyo mkaoni Manyara, Mugasa Mugasa, akizungumzia changamoto za Maabara ya Maandishi