Jumanne , 15th Jul , 2014

Siku moja baada ya Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta, kwa kushirikiana na Makamu Mwenyekiti, Samia Hassan Suluhu, kuteua wajumbe 30 wa kamati ya Mashauriano ,hii leo Viongozi wanaounda Umoja wa Katiba ya wananchi Ukawa wamesema ha

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Dkt Wilbrod Slaa.

Akiongea leo jijini Dar es salaam,Katibu mkuu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ambacho ni miongoni mwa chama kinachounda umoja huo,Dkt Wilbroad Slaa amesema viongozi wanaounda UKAWA hawapo tayari kushiriki mashauriano hayo kutokana na uhalali wa Mwenyekiti wa Bunge hilo kuunda kamati hiyo.

Dkt, Slaa amesema ili kunusuru mchakato huo wa kuundwa kwa katiba mpya Rais Jakaya Kikwete aingilie kati kwa kuunda tume mpya ya kuratibu maoni au tume ya Warioba ikusanye maoni upya kutoka kwa wananchi

kamati hiyo ina wajumbe 30 na Miongoni mwao Wajumbe wa UKAWA walioteuliwa katika tume hiyo ni pamoja na Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe. Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Prof. Ibrahim Lipumba