Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika Magharibi na Kati wa Amnesty Alioune Tine.
Tamko hilo limekuja ikiwa ni karibu miaka miwili tangu serikali ya nchi hiyo iendeshe operesheni ya ukandamizaji dhidi ya washukiwa wa kundi la Boko Haram lenye makao yake nchini Nigeria, na limeitaka serikali ya Cameroon kutoa majibu.
Amnesty imesema kuwa Disemba 27, 2014 maafisa waliwakamata watu zaidi ya 200 kutoka vijiji vya Magdene na Double katika mkoa wa Kaskazini, kama sehemu ya juhudi za serikali kukabiliana na Boko Haram, siku chache baada ya mashambulizi ya ndege za serikali kuwafurusha karibu wapiganaji 1000 wa kundi hilo waliokuwa wameteka kituo cha kijeshi na kushambulia vijiji kadhaa kwenye mpaka wa nchi hiyo na Nigeria.
Shirika hilo limesema linawachukuliwa watu 130 kuwa waathirika wa utoweshwaji wa lazima, jambo ambalo ni kosa chini ya sheria ya kimataifa.
Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika Magharibi na Kati wa Amnesty Alioune Tine, ameitaka serikali kuacha kutumia kisingizio cha mapambano dhidi ya Boko Haram kuhalalisha ukiukaji wake wa wazi wa haki za binadaamu.





