Jumatano , 14th Sep , 2016

Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Mohamed Mpinga ameagiza vyombo vya moto nchini kote zikiwemo bajaji kufanyiwa ukaguzi na uhakiki wa ubora na sifa za kuweza kutembea barabarani ili kuepusha ajali.

Moja kati ya ajali za barabarani ambazo zimekuwa zikitoa nchini

Zoezi hilo litaendana na utoaji wa stika za usalama barabarani kwa vyombo vitakavyothibitika vina ubora wa kutembea barabarani.

Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa wiki ya usalama barabarani Kamanda wa Polisi DCP Mohamed Mpinga amesema magari yatakayobainika kuwa mabovu hayataruhusiwa kufanya shughuli za usafirishaji.

Aidha, wadau wa usalama barabarani wamesema ajenda ya kimataifa kwa nchi zinazoendelea kama ilivyopitishwa katika azimio la kimataifa la muongo wa utekelezaji wa vitendo vya usalama barabarani wa mwaka 2011 hadi mwaka 2020 haina budi kutekelezwa kikamilifu kwani ajali ni miongoni mwa chanzo cha umasikini.